Psalms 142

Maombi Ya Kuokolewa Dhidi Ya Watesi

(Utenzi Wa Daudi. Alipokuwa Pangoni. Maombi)


1 aNamlilia Bwana kwa sauti,
nainua sauti yangu kwa Bwana anihurumie.

2 bNamimina malalamiko yangu mbele zake,
mbele zake naeleza shida zangu.


3 cWakati roho yangu inapozimia ndani yangu,
wewe ndiwe unajua njia zangu.
Katika njia ninayopita
watu wameniwekea mtego.

4 dTazama kuume kwangu na uone,
hakuna hata mmoja anayejihusisha nami.
Sina kimbilio,
hakuna anayejali maisha yangu.


5 eEe Bwana, nakulilia wewe,
nasema, “Wewe ni kimbilio langu,
fungu langu katika nchi ya walio hai.”

6 fSikiliza kilio changu,
kwa sababu mimi ni mhitaji sana;
niokoe na wale wanaonifuatilia,
kwa kuwa wamenizidi nguvu.

7 gNifungue kutoka kifungo changu,
ili niweze kulisifu jina lako.

Ndipo wenye haki watanizunguka,
kwa sababu ya wema wako kwangu.
Copyright information for SwhKC